Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 6 October 2015

ZIPATE HIZI SABABU DK SLAA KUTOONEKANA TENA KWENYE MIKUTANOSiku chache zilizopita kulikuwa na taarifa za kuhusu Dk Wilbroad Slaa kushiriki katika kampeni za chama cha ACT- Wazalendo kwa lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi nchini.


Sasa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba anasema kuwa ni kweli Dk. Slaa ilikuwa afanye nao mikutano ya kampeni katika maeneo tofauti ya Tanzania

"Dk. Slaa alikuwa aanze na Mkutano wa hadhara Mjini Iringa siku ya Jumatano tarehe 7 Oktoba 2015, na baadaye angeendelea na mikutano mingine katika majimbo mbalimbali na kuhitimisha kampeni hizo katika Viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, ambao ndio uwanja ambapo vita dhidi ya ufisadi ilitangazwa rasmi mnamo tarehe 15 Septemba 2007" Alisema Mwigamba

Katibu mkuu huyo wa ACT Wazalendo ameongeza kuwa

Aidha Katibu Mkuu huyo wa ACT - Wazalendo amesema kuwa baada ya tathmini ya kina chama cha ACT-Wazalendo kimejiridhisha kwamba hali ya usalama wa Dk. Slaa ni ndogo sana kwa sasa kutokana na vitisho mbalimbali anavyovipata.

Mwigamba alisema "Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake atakapokuwa majukwaani. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu, chama chetu kimefuta mikutano yote ambayo Dk. Slaa alikuwa aifanye kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo"

Hata hivyo, Mwigamba amesema pamoja na hali hiyo, lakini chama kitaendelea kutambua mchango wa Dk. Slaa katika harakati za kukuza demokrasia na hasa bidii yake ya kujitoa katika kupambana na ufisadi nchini. 

Tunamuahidi kwamba chama chetu kitaendeleza vita hii kwa bidii kubwa na juhudi zake kamwe hazitapotea" . Amesema Mwigamba

No comments:

Post a Comment