Tuesday, 17 November 2015

DALILI HIZI HUASHIRIA MWANAMKE YUPO TAYARI KUPATA UJAUZITO
Kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa baadhi ya wadau wakihitaji kufahamu ni wakati gani mwanamke anakuwa yupo tayari kushika ujauzito.

Leo ninavyo viashiria ambavyo humaanisha mwanamke yupo katika hatari ya kuweza kushika ujauzito yaani 'ovulation period'

Mwanamke kuhisi hamu ya kushiriki tendo la ndoa, wanawake wanapokuwa katika siku zenye uwezekano mkubwa wa kushika mimba basi hata matamanio yao ya kufanya mapenzi huwa ni makubwa zaidi kuliko ilivyo kawaida. Sasa huo ndio wakati unaofaa ikiwa unahitaji kubeba mimba.


Kupanda kwa joto la mwili, hii ni moja ya alama maarufu ambayo hutumiwa na wanawake wengi Ongezeko hilo la joto husababishwa na homoni ya progesterone, ambayo huongezeka sana
mara  baada ya Ovulation.

Kubadilika kwa majimaji ya ukeni, wakati mwanamke anapokuwa katiak uwezekano wa kushika mimba maji ya ukeni nayo huongezeka na kubadilika na kuwa katika hali ya majimaji na wakati mwingine huwa na rangi nyeupe kama  yai bichi. Awali maji hayo ya ukeni huwa na rangi kama ya kream  na hutoka kidogo sana na wengine hushindwa kuyaona kabisa.Maumivu kwenye matiti, baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia kwenye ovulation huwweza kuhisi maumivu kwenye matiti. Hata hivyo njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani maumivu ya matiti huweza kusababishwa na masuala mengine kwani maumivu ya matiti hutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumia baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.

Ikumbukwe kwamba dalili zote hapo juu si lazima zitokee zote kila mwanamke huweza kuona dalili kati ya moja.Kuuelewa vyema mwili wako ni jambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijua siku zako za Ovulation na hivyo kuweza kujua siku zako za kubeba mimba.

Kwa ushauri na maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment