Saturday, 7 November 2015

FAHAMU KUHUSU MIGUU KUPASUKA NA NAMNA YA KUKABILIANA NA HALI HIYO


Kuna baadhi ya watu husumbuliwa sana na tatizo la kupasuka kwa miguu hasa sehemu ya kisigino ambayo hufahamika zaidi kama (magaga au machacha)

Leo Jumamosi napenda kukushirikisha mambo kadhaa kuhusu tatizo hilo la kupasuka miguu.
.

Kimsingi ni kwamba ngozi zetu kawaida huhitaji kuwa na unyevunyevu ambao husaidia ngozi kuvutika au kutanuka pamoja na kusinyaa bila ya kutokea madhara yoyote ikiwemo hili la kupasuka.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mtu apasuke visigino ni pamoja na na hii ya ngozi kuwa kavu sana na hivyo kuifanya ishindwe kutanuka au kusinyaa na hivyo kupelekea ipasuke.

Kuiweka miguu katika maji kwa muda mrefu na baadae kutoipaka mafuta ya kulainisha ngozi, hii huchangia ile asili ya ngozi pamoja na mafuta katika ngozi yapotee na kuiacha ngozi ikiwa kavu sana.

Lakini baadhi yao hukumbwa na tatizo hili kutoka uzito mkubwa wa mwili, jambo ambalo husababisha presha kubwa iwe katika miguu pindi mhusika anapokanyaga chini na endapo ngozi haitakuwa na uimara wa kutosha husababisha visigino kupasuka.

Sababu nyingine ni pamoja na upungufu wa virutubisho muhimu ndani ya mwili mfano madini ya 'zinc' na vitamin E hii nayo husababisha ngozi kupoteza uimara wake na kuifanya ipasuke.

Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na uvaaji wa viatu ambavyo nyuma vipo wazi kwani viatu hivyo huulazimisha mguu au kisigino kutanuka zaidi na hivyo kuuweka mguu hatarini kupasuka.

Pia baadhi ya magonjwa kama vile kisukari nayo huweza kuchangia tatizo hili, lakini pia hata umri mkubwa huweza kuwa sababu ya tatizo hili.

Pamoja na hayo yote, lakini pia tatizo hili huweza kuepukika kwa kuzingatia usafi wa miguu na mwili kwa ujumla, lakini pia kuepuka kutembea sehemu zisizo sawa, rough surfaces, bila kuvaa viatu, hii itaepusha miguu kupasuka.

Ikiwa tayari miguu yako imeshapasuka basi unaweza kuifanyia usafi kisha tumia mafuta ya nasi kupakaa sehemu zenye mipasuko na uzingatie kuvaa soksi na viatu vya kufunika miguu ili kutengeneza unyevunyevu zaidi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment