Thursday, 5 November 2015

FAHAMU KUHUSU UMUHIMU WA VYAKULA VYA WANGA NA PROTINI MWILINI

Njegere hizi huingia kwenye kundi la protini
Ni kweli kwamba kuna aina mbalimbali ya vyakula ambavyo huwa tunakula katika maisha yetu ya kila siku bila kujali faida zake wala madhara yake hii ni kwa sababu wengi wetu tunakula kile tunachokipata na si tunachopenda kula yaani unaweza kusema tunakula kutokana na majaaliwa ya mwenyezi Mungu.

Lakini ukweli ni kwamba chakula unachokula leo ndio afya yako ya kesho hivyo kuna umuhimu mkubwa kuupatia mwili virutubisho vyote muhimu ili kuwa na afya bora. 
Vyakula vimegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na kazi zake mwilini. 

Kwa kawaida mtu anatakiwa kula mchanganyiko wa vyakula vya aina mbalimbali ili kuuwezesha mwili kupata virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika ndani ya mwili.

Leo napenda kukufahamisha hizi aina mbili za makundi ya vyakula pamoja na faida zake


Vyakula vya Wanga. 
Hivi ni vyakula muhimu sana katika mwili kwani huupatia mwili nguvu. vyakula vyenye wanga ni pamoja na mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele n.k. Wanga pia hupatika kupitia viazi vitamu, magimbi, ndizi na hata asali .

Viazi vitamu ambavyo vipo kwenye  kundi la wanga

 Vyakula vyenye Protini  
Hivi ni vyakula muhimu sana katika kujenga mwili pamoja na kusaidia kujenga kinga za mwili. Vyakula vyenye protini ni pamoja na samaki, mayai, maziwa, maharage, soya, kunde, njegere, choroko, mbaazi na hata njugu mawe.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kila wakati kwani tutaendela kukuletea muendelezo wa makundi mengine ya vyakula pamoja na faida zake mwilini. Tafadhari endelea kuperuzi tovuti yetu hii mara kwa mara kadri uwezavyo ili kupata taarifa zaidi kila siku.
 

Kama unaswali kwa Tabibu Abdallaha Mandai basi unaweza kumpigia simu kwa namba zifuatazo 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment