Thursday, 26 November 2015

FAHAMU UMUHIMU WA TUNDA LA PARACHICHI KWA AFYA ZA WATOTO WADOGO


Matunda ni muhimu kwa kilamwanadamu si kwa watu wazima tu bali hata watoto wanahitaji matunda ili kukua vizuri na kuendelea kuwa na afya bora.

Hivyo basi parachichi ni mojawapo ya tunda muhimu pia kwa watoto kwani linavirutubisho vyote muhimu hususani kwa watoto.

Miongoni mwa faida za parachichi kwa mtoto ni pamoja na kumpatia mtoto vitamini nyingi pamoja na madini na miongoni mwa vitamin hizo ni pamoja na vitamin C, A, E na vitamin B-6 pamoja na madini kama vile calcium, iron, magnesium, 'potassium', 'zinc', 'phosphorous' na 'sodium' ambayo yote hayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya afya ya mtoto.

Aidha, matumizi ya tunda la parachichi kwa mtoto husaidia sana kuboresha afya ya macho na akili ya mtoto,.

Pia matumizi ya parachichi husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula kwa mtoto na hivyo kumuepusha dhidi ya tatizo la kukosa choo, lakini pia husaidia kuondosha maumivu madogomadogo ya tumbo na ili kupata faidia zaidi ni nzuri ukapata juisi yake.

Matumizi ya mara kwa ara ya parachichi husaidi sana kulinda afya ya ini kwa watoto na hivyo kumuepusha mtoto dhidi ya magonjwa ya ini pamoja nan moyo.

Tunda la parachichi ni moja ya tunda nzuri sana kwa afya ya ngozi kwani huifanya ngozi kuonekana nyororo na kubaki na uhalisia wake.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment