Monday, 9 November 2015

HAITOSHI KUKWAMBIA UMUHIMU WA PARACHICHI PEKEE NIMEONA KUNA HAJA YA KUJUA NA UMUHIMU WA MAJANI YAKE PIA KATIKA TIBA


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com naamini kwamba utakuwa upo vizuri.

Kama utakuwaa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii naamini utakuwa kuna mengi umeendelea kujifunza kuhusu elimu ya mimea tiba inyotolewa hapa kila siku chini Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic Tabibu Abdallaha Mandai.

Kama ilivyo kawaida yetu kila siku tunakuwa na mambo mbalimbali  ya kuhusu mimea tiba na leo nimeona tuzungumze kuhusu majani ya parachichi.

Wengi tunayafahamu majani haya ya parachichi, lakini si wengi tunafahamu kama yanweza kutumika kama tiba.

Sasa taarifa ni kwamba majani haya yanapochemshwa kama chai na kunywewa husaidia sana kwa wale wenye matatizo ya mwili hususani hali ya kuhisi uchovu na udhaifu.

Tunda la parachichi
Pia unapotafuna majani hayo ya parachichi husaidia sana kutibu matatizo ya vidonda vya mdomoni (ufizi), lakini pia huimarisha meno na kuondoa maumivu. Kwa kifupi tunaweza sema majani haya ni mazuri kwa afya ya kinywa.

Aidha matumizi ya majani au matawi ya parachichi husaidia sana kutuliza maumivu ya tumbo pamoja na matatizo ambayo huambatana na hali ya ubaridi.

Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwa Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment