Wednesday, 25 November 2015

HAKIKISHA HUPITWI NA HIZI FAIDA ZA BILINGANYA KIAFYA..SOMA HAPA UFAIDIKE


Bilinganya ni aina ya mboga ambayo inapatikana katika kundi la mbogamboga, lakini si mboga tu bali nayo inafaida zake kiafya.

Mandai Herbalist Clinic imani yetu ni kwamba kila kitu kilichopo chini ya jua ni baraka ya mwenyezi Mungu na kinafaida yake kwetu sisi binadamu.

Kwa leo nimeona nikwambie hizi faida kadhaa za bilinganya kwako ni vyema ukazifuatilia hapa. Karibu>>

Kwanza matumizi ya bilinganya huwasaidia wale wenye shida ya kisukari kutokana na kwamba bilinganya zina 'carbohydrates' na soluble 'fiber' hivi vyote vinapopatikana ndani ya mwili basi husaidia sana kurekebisha kiwango cha sukari ndani ya mwili hususani kwa wenye kisukari type 2

Hulinda afya ya moyo, bilinganya inasifa ya kulinda afya ya moyo na kumsaidia mhusiaka kuepuka matatizo mbalimbali ya moyo. Bilinganya husaidia sana kuondosha cholesterol mwilini na kusimamia msukumo wa damu kuwa vizuri mwilini.

Pia matumizi ya bilinganya husaidia sana kuongeza madini chuma mwilini pamoja na kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na kuondosha matatizo ya kukosa choo.

Pamoja na hayo. inaelezwa kuwa matumizi ya bilinganya mara kwa mara huwasaidia wale watu wanaovuta sigara na wanahitaji kuacha kuvuta sambamba na kupambana na magonjwa sugu kama vile kiharusi  na hayo matatizo ya moyo.

Ndani ya bilinganya kuna 'antioxidants' ambayo husaidia sana kupambana na maambukizi ya saratani.


Hayo ni machahe tu lakini kwa maelezo zaidi au kama unasumbuliw na tatizo lolote la kiafya wasiliana na Tabibu Abdallah Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

1 comment:

  1. Doctor mi natatizo la kukoswa usingizi nitumie tiba gani asili

    ReplyDelete