Monday, 30 November 2015

HIKI NDIO KILEVI AMBACHO HUSABABISHA WANAUME KUSHINDWA KUFANYA VIZURI KITANDANI

Utafiti uliofanywa kwa niaba ya serikali ya Kenya na wahadhiri wa chuo kikuu cha Moi kilichoko katika Bonde la ufa umebaini kuwa Majani ya miraa inayofahamika pia kama 'Mirungi' unazuia ukuaji wa manii.

Aidha ulaji wa kipindi kirefu wa miraa unafanya mbegu za kiume za wanaume kufa haraka pindi zinapowekwa kwenye uke.

Mtafiti mkuu wa chuo kikuu cha Moi, Ochiba Lukanda, anasema kuwa utafiti sawa na huo uliofanywa huko ghuba ulibaini matokeo kama hayo.

Lukanda anasema kuwa wanaume ambao wanakula miraa kwa kipindi kirefu na wakaacha huwa wanapata uwezo wao wa kutunga mimba.

Ulaji wa Miraa pia huwa unasababisha mshtuko wa moyo.''Mtu anapokula mmea huu baada ya muda damu yake huaanza kwenda kwa kasi, mbali na shinikizo la damu mumea huu hausababishi saratani kama inavyodaiwa '' Dakta Lukanda

Naye daktari Lukoye Atwoli alisema kuwa miraa husababisha walaji wake kuwa na mori na hata wakati mwengine msongo wa mawazo.

Utafiti huu unafwatia ule uliofanywa mwaka uliopita na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Konstanz cha Germany na kile cha Minnesota, Marekani uliobaini kuwa ulaji wa miraa unaathiri ubongo wa walaji wake na kusababisha msongo wa mawazo,mafadhaiko na mahangaiko ya kiakili mbali na matatizo mengine chungu nzima.

No comments:

Post a Comment