Tuesday, 24 November 2015

HIZI NDIO SABABU AMBAZO ZITACHANGIA KUPATWA NA SHINIKIZO LA DAMU

Shinikizo kubwa la damu hutokea wakati damu yako inatiririka kupitia mishipa yako na kusababisha mgandamizo mkubwa katika kuta za mishipa ya damu, mgandamizo ambao ni mkubwa kuliko ule wa kawaida.
Miongoni mwa chanzo cha mtu kupata shinikizo kubwa la damu ni kama hivi vifuatavyo:

• Chakula chenye kiwango kikubwa cha mafuta na hasa mafuta yatokanayo na wanyama, cholesterol

• Mwili kutofanya mazoezi, au kutofanya mazoezi katika kiwango kinachotosheleza,

• Kuwa na uzito mkubwa wa mwili, (overweight)

• Historia ya familia kuwa na shinikizo la damu,

• Matumizi ya tumbaku,

• Msongo wa mawazo, 'stress'

• Baadhi ya dawa zinazotumika katika kutibu magonjwa

• Matatizo ya figo na homoni.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment