Friday, 20 November 2015

IPATE HII SIRI NYINGINE YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MATIBABU


Typhoid ni miongoni mwa magonjwa ambayo hujumuishwa kwenye kundi la magonjwa ya homa ya matumbo.

Ugonjwa huu ni matokeo ya mhusika kula chakula au kunywa maji yaliyochafuliwa kwa haja ndogo au kinyesi cha mtu mwenye ugonjwa huo.

Vimelea wanaoeneza ugonjwa huu wanafahamika kama salmonella typhi na mara nyingi mgonjwa anapopata maambukizi basi huanza kuziona dalili baada ya wiki ya kwanza au wiki ya tatu, ambapo mgonjwa huanza kuwa na homa, kuumwa kichwa, kuharisha na maumivu ya tumbo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa kila mwaka  watu 222,000 wanakufa kati ya milioni 21wanaougua ugonjwa wa homa ya matumbo.

Kuna baadhi ya sababu ambazo huchangia sana kuenea kwa ugonjwa huu ambazo ni pamoja na hali ya mazingira duni ya kimaisha pamoja na kutozingatia kanuni za usafi.

Kuna baadhi ya dawa ambazo mgonjwa wa tatizo hili hupatiwa anapofika hospitali na kuweza kuwa vizuri, lakini pia unaweza kutumia njia hii ya asili ya kukabiliana na tatizo hiki la homa ya matumbo yaani typhoid.

Njia hiyo ni matumizi ya kitunguu swaumu kwani huweza kuua bakteria wanaosababisha ugonjw ahuo na unachopaswa kufanya ni kutafuna punje mbili kila siku asubuhi na jioni hadi pale utakapoona mabadiliko.

Kumbuka kwamba ukiona huoni mabadiliko ni vyema kufika kwa wataalam kwa ushauri zaiidi au mpgine Tabibu Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0784 300 300

ZINGATIA: MATUMIZI YA KITUNGUU SWAUMU KWA MAMA MJAMZITO NA ANAYENYONYESHA NI HATARI HIVYO MAKUNDI HAYO HAYAPASWI KUTUMIA KITUNGUU SWAUMU

No comments:

Post a Comment