Monday, 2 November 2015

JE, UNAIJUA NCHI AMBAYO HUPEPERUSHA BENDERA YA TAIFA NUSU MLINGOTI KILA ANAPOFARIKI RAIA WAO?

Bendera ya Iceland
Ishu ya bendera ya taifa kupeperushwa nusu mlingoti si jambo la kawaida kabisa katika nchi nyingi na inapotokea hali hiyo basi huwa kunasababu ya msingi sana ikiwa ni pamoja na kifo cha kiongozi mkubwa serikalini au kuna janga la kitaifa ambalo litakuwa limesababisha maafa kwa wananchi wengi.

Kutokana na hali hiyo basi jamii nyingi au nchi nyingi zinaamini kuwa bendera ya taifa huwa haipeperushwi ovyo bila sababu maalum na ya msingi, lakini jambao la kushangaza ni hii stori kutoka mji mmoja wa kaskazini mwa Iceland ambao wao utaratibu wao ni tofauti kidogo kwani wamekuwa wakipeperusha bendera ya taifa nusu mlingoti kila mkazi wa mji huo anapofariki.

Hata hivyo, madiwani wa mji huo wa Husavik wenye wakazi 2,000 wameamua kusitisha utamaduni huo wa kupeperusha bendera ya taifa kila kinapotokea kifo cha mkazi wa mji huo wakidai kwamba utamaduni huo sasa haufai kwa sababu wakazi hawajuani kama ilivyokuwa zamani.

Maelfu ya watu huzuru Husavik kutazama nyangumi
Kwa mujibu wa gazeti la Morgunbladid lilieleza kuwa mji wa Husavik ni mji wa kitalii na huvutia sana watu wanaofika kutazama nyangumi, ambapo diwani mmoja kutoka eneo hilo Hjalmar Bogi Haflidason anasema kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti huwashangaza sana watalii.

“Wengi huwa wanadhani kiongozi wa nchi amefariki,” anasema.

Pamoja na hayo, mmoja wao Sofia Helgasdottir aliiambia tovuti ya Visir kuwa: "Huu ni utamaduni ulioanza zamani na tumekua nao. Ninafikiri ni utamaduni mzuri sana.” huku akiongeza kuwa kuhusu wageni kushangazwa, amesema wageni hao ndio wanaofaa kujifunza tamaduni za wenyeji.

No comments:

Post a Comment