Monday, 2 November 2015

JIFUNZE NAMNA YA KUONDOA MADOA YA CHUNUSI USONI KWA KUTUMIA JUISI YA LIMAO NA VIAZI
Vijana wengi wanapofika umri fulani wa kupevuka kiakili hukumbwa na tatizo la chunusi kiasi ambacho huwakera na kuwakosesha raha kabisa.

Lakini siku ya leo sina lengo la kuzungumza kuhusu tatizo la chunusi leo nataka kueleza kuhusu yale mabaka meusi ambayo hubaki kwenye ngozi mara baada ya kuisha kwa chunusi.

Ni kweli kwamba yale mabaka meusi au kwa lugha ya wenzetu yaani kingereza hufahamika kama 'black spots' hukosesha raha kabisa na hata kupoteza muonekano wa muhusika pia.

Hapa ninazo baaadhi ya njia  ambazo ukifanya husaida sana kuondosha tatizo hilo la mabaka meusi yatokanayo na kupona kwa chunusi.

Juisi ya  Limao
Hii juisi ni mojawapo ambayo huweza kuondosha mabaka kwenye ngozi yako kutokana na juisi hii kuwa na kiwango kingi cha vitamin C ambayo husaidia kufubaza yake madoa meusi kwenye ngozi yako.

Unachopaswa kufanya ili kutumia juisi hii ya limao kama tiba utatakiwa kuandaa juisi hiyo ya limao kisha tafuta kipande cha pamba.

Baada ya kuandaa hivyo utachukua kipande cha pamba na kuchovya kwenye juisi ya limao kisha utapaka moja kwa moja kwenye sehemu iliyoathirika yaani sehemu yenye baka jeusi au mabaka meusi.

Baada ya kupaka juisi hiyo ya limao utakaa nayo kwa dakika kadhaa kisha utaosha uso wako kwa maji safi na salama. Utaendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo na utaanza kuona mabadiliko ya ngozi yako.

Viazi Mviringo
Hivi viazi hutumika kwa kukata kata katika vipande vidogo vya mviringo 'slice' kisha utaweka kipande hicho ile sehemu yenye tatizo yaani yenye baka nyeusi na utaiacha hapo kwa muda wa dakika kadhaa kisha utanawa kwa maji safi yenye umoto kiasi.

Viazi mviringo
Kwa maelezo zaidi au ushauri wasiliana  na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


1 comment: