Friday, 20 November 2015

JINSI MDALASINI UNAVYOWEZA KUMSAIDIA MTOTO MWENYE TATIZO LA KUKOJOA KITANDANI


Tatizo la kukojoa kitandani ni miongoni mwa matatizo yanayo wakabili watoto wengi kwenye baadhi ya familia.

Kukojoa kitandani ni ile hali ambayo hutokea mhusika anajikuta akitoa haja ndogo akiwa usingizini pasipo yeye mwenyewe kufahamu.

Mzazi unaweza kujiridhisha kuwa mtoto wako anasumbuliwa na tatizo hili mara unapoona mtoto amefikisha umri wa miaka sita na bado anakojoa kitandani basi ujue tayari mtoto anatatizo hilo.

Hata hivyo, ni vyema ikafahamika kuwa watoto wenye tatizo hili si kwamba hupenda kukojoa kitandani bali ni matatizo yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kibofu cha mkojo. Hivyo mwanao anapokuwa na tatizo hili usimdharirishe kwa kumtembeza mtaani huku akiimbiwa na watoto wenzie hali hii huweza kuchangia mtoto kuathirika kisaikolojia na baadaye akashindwa kabisa kuchangamana na jamii katika kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.

Watoto wengine hukumbwa na tatizo hili kufuatia kulala fofo kwa sababu ya kuchoka sana mchana kutokana na michezo yao, hali ambayo husababisha akili kushindwa kupokea taarifa kuwa kibofu kimejaa na haja ndogo inahitajika kutolewa.

Pamoja na hayo yote kuna baadhi ya vitu ambavyo tupo navyo karibu kabisa kwenye maisha yetu ya kila siku ambavyo vikitumika vizuri huweza kuwa msaada kwa tatizo hili, mojawapo ni mdalasini.

Mdalisini unauwezo mzuri wa kumsaidia mtoto mwenye tatizo hili la kukojoa kitandani jambo la kufanya ni mzazi kumpatia mtoto wako kipande (gome) moja la mdalasini atafune kila asubuhi mchana na jioni kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu mfululizo.

Mbali na mdalasini pai unaweza kumpatia mtoto mwenye tatizo asali kijiko kimoja kila siku kabla ya kulala.

Kwa ushauri zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail,com

No comments:

Post a Comment