Monday, 30 November 2015

JINSI UNAVYOWEZA KUEPUKA MATATIZO YA MOYO KWA KUFANYA MAZOEZI YA KUKIMBIA TU.!Mara kadhaa tumekuwa tukiambiana kuhusu umuhimu wa mazoezi kwa afya zetu moja ya faida kubwa ya mazoezi ni pamoja na kujilinda dhidi ya magonjwa hususani yale yasiyoambukiza.

Leo nimeona nikwambie huu umuhimu wa mazoezi ya kukimbia kwani nayo huwa na faida zake katika miili yetu.

Kwanza kabisa unapofanya mazoezi ya kukimbia tambua kwamba unatengeneza mazingira mazuri na bora kwa afya ya moyo wako, kwani kitendo cha kukimbia humfanya mhusika kupumua kwa nguvu na hivyo kufanya moyo kufanya vizuri kazi yake ya kusukuma damu mwilini.

Likini pia mazoezi ya kukimbia husaidia mzunguko wa damu mwilini kuwa vizuri hivyo mazoezi ya mara kwa mara yanahitajika zaidi ili kubaki kuendelea kuwa na afya bora zaidi.

Kufanya mazoezi ya namna hii pia husaidia sana kupunguza uzito wa mwili kwa mhusika  hii ni kwa sababu unapokimbia mwili unakuwa unaunguza calories na hivyo kumfanya mhusika kupungua kadri siku anazokuwa akifanya mazoezi.

Mazoezi pia hupunguza msongo wa mawazo, tatizo hili si la kulipuuza hata kidogo kwani ni moja ya sababu ya magonjwa kadhaa yasiyoyakuambukiza na huweza kusababisha vifo sasa ili kuepukana na hayo masuala ya kuzongwa kimawazo unahitaji kufanya mazoezi ambayo yatakufanya kujihisi mwenye amani .

Mbali na hayo, mazoezi pia husaidia sana kuongeza umakini kwa mhusika 'concentration' na hivyo kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment