Tuesday, 10 November 2015

JINSI YA KUPAMBANA NA VIDONDA VYA TUMBO


Vidonda Vya Tumbo
Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaotokea kutokana ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba kutengeneza kidonda/vidonda.

Ukuta wa tumbo huwa unatoa gastriki yenye mchanganyiko wa asidi ya haidrokloriki na vimenyenyo. Unapopata hamu ya kula au wakati unakula asidi hii huzalishwa na tumbo ili kumenyenya chakula. Ukuta wa tumbo hufunikwa na layer ya mucus ambayo huzuia asidi hii isitoboe ukuta wa tumbo au utumbo mdogo.

Vidonda hivyo vya kwenye utumbo huweza kutokana na kutokula kwa wakati, maambukizi ya Helictobacter pylori, kuvuta sigara au matumizi holela ya madawa za kutuliza maumivu. asidi huzalishwa zaidi na hivyo kukwangua ukuta wa tumbo au utumbo mwembamba na vidonda kutokea.

Jinsi ya kuishi na vidonda vya tumbo.
Acha kutumia kahawa na chai, kwa maana vitu hivi huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa na tumbo lako. Unaweza tumia chai ya mitishamba Mfano mchaichai

Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.

Epuka matumizi ya vileo kwani unywaji wa pombe mara kwa mara huweza kutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.

Kama ni mvutaji wa sigara basi acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone.

Kama tayari unasubuliwa na tatizo hili wasiliana na Tabibu Abdallaha  Mandai kwa simu 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment