Wednesday, 18 November 2015

KAMWE USIPUUZE MAUMIVU YA KIFUA HUWEZA KUWA NI KIASHIRIA CHA MATATIZO MENGINEKuhisi maumivu ya sehemu ya kifua ni moja ya tatizo ambalo halipaswi kuchukuliwa mzaha hata kidogo na pindi hali hiyo inapotokea ni vyema kutafuta ufumbuzi wa shida hiyo.

Miongoni mwa sababu ambazo huweza kusababisha mhusika kuhisi maumivu sehemu ya kifuani ni pamoja na uvutaji wa sigara, kisukari, uwingi wa mafuta hatari kwenye mishipa ya damu ' cholesterol' shinikizo la juu la damu au huweza kuchangiwa na historia ya magonjwa ya moyo kwenye familia.

Ili kutibu tatizo hili huhitaji kuonana na wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi, lakini pia kuna njia hii ambayo unaweza kujaribu kabla ya kuamua kuoanana na daktari wako.

Maumivu ya kifua huweza kutulizwa kwa kutumia tangawizi, hii ni kwa sababu tangawizi huwa na uwezo mzuri wa kuondosha au kupunguza mafuta hatari yaani cholesterol lakini pia husaidia mishipa ya damu kutoharibiwa na cholesterol.

Sasa unachopaswa kufanya ili kutumia tangawizi kama tiba ya tatizo hili andaa kiasi cha kikombe kimoja cha tangawizi kunywa.
Ni nzuri upate tangawizi ambayo haina majani ya chai

Je, unahitaji maelezo zaidi? basi usisite kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment