Tuesday, 10 November 2015

KENYA NAO WAMEAMUA KUTORUHUSU BODABODA KUINGIA KATIKATI YA JIJI (VIDEO)


Ishu ya madereva bodaboda na bajaji kuzuiwa kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam ni moja ya mambo ambayo kwa sasa yameshazoeleka kabisa, sasa taarifa kama hii imeigusa Nairobi nchini Kenya bodaboda wa nchi hiyo nao kupigwa marufuku kuonekana mjini wakisafirisha wateja wao.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoripotiwa na Kituo cha Tv cha K24 madereva bodaboda wameonekana kuipokea vibaya taarifa hiyo na kusema kwamba wanazuiwa kuingia mjini lakini hawajaoneshwa wapi ni eneo rasmi kwao kwa kufanya shughuli zao za usafirishaji

Hata hivyo, agizo hilo linasema kwamba hata endapo bodaboda itakamatwa ikikatisha katikati mwa jiji hilo basi abiria pamoja na dereva wote kwa pamoja watawajibishwa kwa kulipa faini.

Unaweza kupata undani wa taarifa hii kupitia video hii hapa chini>>>>

No comments:

Post a Comment