Thursday, 26 November 2015

LEO NAKUPATIA HIZI FAIDA NZURI ZA KIAFYA ZA JUISI YA BOGA

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com imani yangu kwamba unaendelea vizuri popote pale ulipo unaposoma makala hizi fupi.

Tayari tumewahi zungumza mara kadhaa kuhusu boga, lakini leo napenda tuzungumze kuhusu boga lakini tuangalie faida za juisi yake.

Najua kwa baadhi ya watu itakuwa ni jambo la kushangaza kusikia kuhusu juisi ya boga lakini hakuna kitu ambacho kinashindikana chini ya jua.

Zipo faida kadhaa za matumizi ya boga na hapa napenda kukufikishia hizi baadhi>>>>>>

Juisi ya boga inauwezo mzuri wa kupambana na shinikizo la juu damu pale unapokunywa mara kwa mara hii ni kwa sababu ndani ya boga kuna kirutubisho kiichacho 'pectin' ambayo hufanya kazi kubwa ya kushusha cholesterol na hivyo kupambana na matatizo ya shinikizo la damu.

Huimarisha kinga za mwili, juisi ya boga ina virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini pamoja na vitamin, ambavyo ni muhimu sana kwa kuimarisha kinga za mwili ndani yetu.

Juisi ya maboga haisaidii tu shinikizo la damu na kuimarisha kinga za mwili bali husaidia sana kumkinga mhusika dhidi ya matatizo ya shambulio ya moyo pamoja na kiharusi 'stroke'

Aidha, matumizi ya juisi hii ni muhimu sana kwa afya ya figo na ini katika hili juisi hii itakusaidia zaidi pale unapokunywa mara tatu kwa siku yaani asubuhi mchana na jioni kila siku kwa kufanya hivyo husaidia sana hata kuondosha mawe kwenye figo.

Pamoja na hayo, juisi hii ni nzuri sana kwa kurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni, 'digestion system' kutokana na kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi  'fiber' za kutosha hivyo juisi hii ni kinga tosha ya matatizo kukosa choo mara kwa mara.

Ndugu msomaji wangu hizo ni faida kadhaa za matumizi ya juisi ya boga, napenda kukuahidi kwamba bado ninazo faida nyingine za juisi hii ya boga endelea kutembelea tovuti hii mara kwa mara ili kuayafahamu mengine mengi kuhusu faida hizi.

Hata hivyo, kama utakuwa na swali au maoni unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment