Monday, 16 November 2015

MAAMUZI MENGINE YA HOSPITALI YA MUHIMBILI KUHUSU KUSITISHA HUDUMA ZA MRI NA MATENGENEZO YA CT- SCANIkiwa ni siku chache baada ya mashine za MRI kuanza kufanya kazi katika hospitali ya Taifa Muhimbili, taarifa mpya ni kwamba uongozi wa hospitali hiyo umeamua kusitisha huduma hizo kwa muda kuanzia leo kwa ajili ya matengenezo.

Awali mashine hizo zilianza kufanya kazi baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kukuta mashine zote mbili za MRI na CT Scan zikiwa mbovu

Itakumbukwa baada ya ziara hiyo ya Rais wiki iliyopita huduma za MRI zilianza kufanya kazi baada ya mashine hiyo kutengenezwa lakini siku chache zilizopita ilionekana kuwa na hitilafu ya kiufundi ambayo inahitaji matengenezo.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Aminiel Eligaesha amesema tayari uongozi wa hospitali unawasiliana na kampuni iliyopewa kazi ya kutengeneza ili kurekebisha hitilafu hizo.


No comments:

Post a Comment