Wednesday, 11 November 2015

MAFUTA YA KARAFUU NI TIBA TOSHA YA MAUMIVU YA KICHWA, JIFUNZE HAPA NAMNA YA KUYATUMIAHivi ni mara ngapi umejikuta ukizongwa na maumivu ya makali ya kichwa? najue huenda hali hiyo itakuwa imewahi kukuta mara kadhaa na usijue nini cha kufanya.

Huenda kuna wakati unajikuta kichwa kinauma sana na hata unapopata dawa za kutuliza maumivu hali inakuwa bado haiko vizuri na ukisema ukapime labda huenda itakuwa ni malaria bado unaambiwa hakuna kitu na badala yake unaishia kuambiwa unywe maji ya kutosha na kupata mapumziko ya kutosha pia.

Lakini leo napenda kukupatia hii tiba nyingine ya asili ambayo unaweza kuifanya ukiwa hapo nyumbani kwako na kujikuta unafanikiwa  kutuliza maumivu ya kichwa si nyingine bali ni matumizi ya mafuta ya karafuu.
headache
Maumivu ya kichwa ni hatari

Mafuta ya karafuu ni msaada mzuri sana wa maumivu ya mwili ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa, unachopaswa kufanya ni kutafuta pamba au tishu ambayo safi kisha chovya kwenye mafuta ya karafuu baada ya hapo chukua hiyo pamba au tishu yenye mafuta ya karafuu kisha weka sehemu ya mbele ya kichwa chako.

Kaa kwa muda wa dakika 15 na hiyo pamba au tishu jambo ambalo huenda kusaidia kuachia misuli ya kichwa iliyokaza na kusababisha maumivu kuanza kupungua.

Ukiona hali inaendelea ni vyema ukafanya utaratibu wa kufika kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe kwaajili ya kuweza kupata msaada zaidi.

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa ushauri au maelekezo zaidi mpigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment