Friday, 6 November 2015

MAJANI YA MNYONYO HUSAIDIA SANA KWA WENYE GANZI YA MIGUU NA KUVIMBA KWA MIGUUNI, FAHAMU HAPA NAMNA YA KUYATUMIA


Mnyonyo ni mojawapo ya mmea unaopatikana sana porini, lakini baadhi ya familia hupanda miti hii pia kando kando ya nyumba zao.

Moja ya mikoa ambayo miti ya minyonyo huweza kushamiri zaidi ni pamoja na mkoa wa Iringa.

Hapa leo napenda kuzungumza kuhusu baadhi ya faida ambazo huweza kupatikani kwa kutumia mmea huu.

Kwanza kabisa unapotumia majani ya mnyonyo kwa kufunga miguu inayouma, ambapo utatumia majani hayo kwa kukanda ile miguu na hayo majani yakiwa yamepashwa moto.

Majani yaliyopondwa yakibandikwa juu ya tatizo la ngozi huweza kuwatiba ya magonjwa ya ngozi

Aidha kwa wale wenye shida ya miguu kufa ganzi na kuwaka moto huweza kutumia mafuta ya mnyonyo kwa ajili ya kuchua miguu.

Zingatia:
Usitumie tiba hii ya mnyonyo bila kuwa na uangalizi wa wataalam wanaofahamu zaidi mimea tiba, hivyo kabla hujaamua kutumia tiba hii wasiliana kwanza na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment