Wednesday, 25 November 2015

MAJANI YA MPAPAI KATIKA TIBA, HUWEZA KUTULIZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHIKuna mimea mingi yenye faida kwa afya zetu ambapo pale inapotumika vizuri huweza kuwa tiba ya magonjwa mbalimbali.

Leo nimeona tuzungumze kuhusu majani ya mpapi, haya ni majani ambayo yanauwezo wa kutibu matatizo yetu kadhaa ya kiafya.

Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na matatizo ya maumivu makali kwa wanawake wakati wa hedhi, unachofanya ni kuchemsha majani hayo na kunywa mara baada ya maji hayo kupoa utakunywa glasi moja kwa kila siku asubuhi na jioni.

Aidha, majani haya ni mazuri kwa wale wenye matatizo ya umeng'enyaji wa chakula na hivyo kurahisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni, lakini pia majani haya yanauwezo wa kuwasaida wale wenye shida ya kukosa hamu ya kula.

Majani ya mpapai ni kinga nzuri dhidi ya magonjwa ya saratani, lakini pamoja na hayo majani haya huweza kuwasaidia wale wenye shida ya chunusi.

Matumizi ya majani ya mpapai husaidia sana kuimarisha kinga za mwili, hii ni pale unapopata juisi yake ya majani hayo basi utakuwa ukiimarisha kinga za mwili wako na kukufanya kujikinga zaidi dhidi ya magonjwa.

Pamoja na hayo, majani haya ya mpapai huweza kupambana dhidi ya malaria, kikubwa unachohitajika kufanya ni kupata juisi ya majani hayo kwa kila siku kiasi cha glasi moja asubuhi na jioni. Jitahidi kunywa kwa muda wa wiki mbili ili kupata mafanikio zaidi.

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment