Monday, 30 November 2015

MAMBO MANNE MUHIMU YA KUYAJUA KUHUSU NANASI, KUANZIA TUNDA LAKE, MIZIZI NA MAUA YAKE


Nanasi ni moja ya tunda ambalo lina ladha nzuri sana kwa waliowengi lakini pia si ladha tu bali tunda hili lina faida zake pia za kiafya.

Hivyo leo bila hiyana nimeona ni vyema nikupe hii orodha ya faida za nanasi kwa ujumla wake kama ifuatavyo:

Kwanza tukianza na juisi ya majani yake ni dawa ya kutibu vidonda na matatizo ya magonjwa ya ngozi na majipu.

Aidha mizizi ya nanasi nayo inapochemshwa huwa ni dawa ya matatizo ya figo na kuua minyoo mwilini.

Halikadharika maua ya nanasi yanapochanganywa na asali huwa ni tiba ya mafua na kikohozi, tumia kijiko kimoja kwa siku.

Nanasi pia huwa ni msaada kwa wale wenye shida ya matatizo ya akili na kupoteza kumbukumbu.

Tunda hili pia husaidia kutibu matatizo ya tumbo, ini, magonjwa ya bandama, homa, pumu pamoja na kusaidia kuongeza maziwa kwa kinama.

Hayo ni machache tu kuhusu nanasi kwa mengine mengi hakikisha unawasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment