Friday, 13 November 2015

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANDA CHAKULA KIAFYA

Chakula kizuri na salama uandaliwa kwa kufuata taratibu zote za kiafya, na siku zote unapokula chakula kilichoandaliwa kwa kufuata taratibu za kiafya lazima utaendelea kubaki kwa na afya njema.

Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia katika uandaaji wa chakula>>>

USAFI
Nawa mikono yako vizuri kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni kabla ya kushika chochote kila inapobidi wakati wa kuandaa chakula hicho.

TENGANISHA VYAKULA VIBICHI NA VILIVYOPIKWA
Vyakula vilivyopikwa kama nyama, samaki, kuku na aina nyingine ya vyakula visichanganywe na vile ambavyo havijapikwa.

Tenganisha vifaa kama kisu na ubao wa kukatia chakula kilichopikwa na kile kisichopikwa Hifadhi vyakula visivyopikwa tofauti ili visichanganywe na vile vilivyopikwa.

PIKA CHAKULA KIIVE
Hakikisha chakula unachopika kinaiva vizuri, kama ni nyama, samaki hakikisha vinaiva vizuri kabisa.Vyakula vinapoiva vizuri husaidia kuua vimelea vya magonjwa.

TUMIA MAJI SALAMA.
Hakikisha maji unayotumia kupikia ni safi na salama na kama unatumia matunda basi yaoshe kwa maji safina salama.

Unaweza kupata maelezo zaidi kupitia kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment