Wednesday, 25 November 2015

MANENO YA MKEMIA MKUU KUHUSU KEMIKALI HATARISHI NA MIKAKATI YAOMkemia Mkuu wa Serikali Samuel Manyele leo amejitokeza mbele ya wandishi wa habari katika ofisi yake, Dar es salaam na kuzungumzia suala zima la kemikali hatarishi zinazoingia nchini kinyume na sheria pamoja na mikakati waliyojiwekea.

Akizungumzia taratibu za uingizwaji wa kemikali nchini Manyele amesema “kila mtu anayetaka kuingiza kemikali nchini lazima apate kibali na kuhakikisha kwamba ni salama kwa afya za wananchi"

Aidha amesema kuwa wameanzisha bandari kavu kwa ajili ya kuhifadhi kemikali hatarishi na kusimamiwa kabla ya kuanza safari ya kwenda kwenye nchi kavu ili kuhakikisha viwango vimezingatiwa na kubainisha kuwa utaratibu huo utarahishisha usimamizi wa kukabiliana na madhara yoyote yatakayoweza kujitokeze.

Kuhusu utolewaje wa vibali  Prof.Samuel Manyele amesema kuna kemikali ambazo ni hatari sana kwa binadamu na haziruhusiwi kuingia nchini..”Hutolewa kwa matumizi ya Serikali tu”.

Akieleza kuhusu kiasi cha kemikali zilizoingia nchini tangu Januari hadi Oktoba 2015 Prof Manyele amesema .“Jumla ya tani zilizoingia kwenye mipaka mbalimbali na bandari jumla ya tani 472,393 za Kemikali ziliingizwa nchini kwa kipindi cha miezi kumi, bandari ya Dar es Salaam ndio inaongoza kwa kuwa na tani nyingi 281,468 ikifuatiwa na Tunduma yenye tani 199, 000, Mtwara, Tanga, Horohoro, Mwanza na Sirari tuna list kubwa inayoonyesha ni kiasi gani kemikali hizo zinapita katika bandari hizo”
Mpaka wa Tunduma unapitisha Kemikali nyingi kutoka Tanzania kwenda nchi za nje na ni 80% ya kemikali hupita katika bandari hiyo.

Pia amezungumzia mikakati ya Serikali ambapo amesema ”Kuongeza watumishi kwa wakala ambao wameanza kupelekwa kwenye mipaka inayoingiza kemikali kwa wingi, kuiwezesha Serikali kufuatilia kemikali hizo kwa ukaribu, Serikali kufanya maamuzi ya ajira kiasi gani zitolewe na tayari watumishi wameanza kusambazwa katika mipaka yote inayoingiza Kemikali hizo” .Prof.Samuel Manyele

Katika kufanikisha ilo Serikali imeandaa mafunzo ya siku mbili yanayoanza kesho ambayo yatakuwa maalum kwa kutoa elimu ya kemikali hizi na yatashirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika Kusini pamoja na Ghana.

No comments:

Post a Comment