Wednesday, 11 November 2015

MANUFAA YA KUTUMIA MAFUTA YA NAZI

Mafuta ya nazi kwa kawaida ni mazuri sana kwa afya ya ngozi kutokana na kutokuwa na kemikali ambazo huweza kuathiri ngozi.

Moja ya matatizo yanayoweza kupata ufumbuzi kupitia mafuta ya nazi ni pamoja na kutibu fangasi za miguuni, ambapo kinachohitajika ni kuchanganya mafuta ya nazi na maji ya mchai mchia kisha tumia maji hayo kupaka sehemu iliyoathirika mara mbili kwa siku hadi pale tatizo litakapo isha.

Husaidia kuondoa madoa na muwasho kwenye ngozi, jambo la kufanya ni kupaka kwenye sehemu iliyothirika mara mbili kwa siku kwa muda wa siku zisizopungua ishirini na moja hivi.

Kwa wale wenye shida ya tatizo la bawasiri au uvimbe kwenye sehemu ya haja kubwa, pia wanaweza kutumia mafuta haya ya nazi kwa muda usiopungua mwezi mmoja kwa kupaka mara mbili kwa siku na tatizo hilo litaisha au kupata auheni.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300.Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment