Tuesday, 17 November 2015

MBEGU YA PARACHICHI NI TIBA YA MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA


Tatizo la kupata haja ndogo (mkojo) yenye kuambata na maumivu makali, huku ikitoka kwa taabu sana hili ni tatizo ambalo huwakumba watu wengi na baadhi yao hushindwa kuelewa sababu ya tatizo hilo.

Kimsingi ni kwamba kupata maumivu wakati wa haja ndogo ni moja ya dalili kuwa mhusika amepatwa na maambukizo kwenye njia ya mkojo (U.T.I) .

Watu wenye tatizo hili hujikuta wakikosa raha na amani kabisa wakati wanapohitaji kupata haja ndogona wengine hufika wakati kutotamani kabisa kupata haja ndogo.

Hata hivyo, maumivu haya huweza kuwa ni dalii ya matatizo mengine mbali na U.T.I kwani huweza kuwa tatizo la tezi dume, kisonono au matatizo ya mawe kwenye figo 'kidney stones'

Lakini tatizo hili pia huweza kuwakumba wale ambao si wapenzi wa kunywa maji ya kutosha, hivyo ni muhimu kuzingatia kunywa maji ya kutosha angalau lita 4 kwa siku ili kukabiliana na tatizo hilo. lakini endapo utakunywa maji ya kutosha na bado tatizo likaendelea  basi ni vyema utumia tiba hii ifuatayo:

Tafuta mbegu au peke la parachichi 'avocado seed' na ulisage kisha kaanga kiasi , baada ya hapo utatumia unga huo kwa kuweka vijiko viwili vya unga huo kwenye kikombe chenye maji ya moto na kukoroga vizuri kisha kunywa maji hayo. Fanya hivyo kwa muda wa siku 10  asubuhi na jioni ili kumaliza tatizo hilo

Unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha  Mandai kwa maelezo zaidi piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment