Thursday, 12 November 2015

MCHANGANYIKO WA ASALI NA MADALASINI UNAVYOWEZA KUWASAIDIA WANAWAKE WENYE MATATIZO WAKATI WA HEDHI

Matatizo ya hedhi yamekuwa yakiwasumbua wanawake wengi, kwani imekuwa ni kawaida sana kusikia kina dada wakilalamika kutoona siku zao na hawana mimba, au wengine kuona siku zao bila mpangilio mzuri wa tarehe na wengine wakibahatika kuona basi hujikuta wakitokwa na damu nyingi kupita kiasi.

Katika hali ya kawaidia mwanamke anapoingia kwenye siku zake hupaswa kuona damu ndani ya siku moja hadi tatu, licha ya kwamba wengine huweza kufika hadi siku saba.

Shida inakuja pale ambapo mwanamke anaona siku zake, lakini  damu zinatoka nyingi kupita kiasi hata pale wanapovaa 'pad' zinachafuka haraka sana kwa muda mfupi na humlazimu mwanamke kubadilisha mara nyingi zaidi ya ilivyo kawaida.

Tatizo hili la kutokwa na damu nyingi kupita kiasi wakati wa  hedhi huwa na sababu nyingi na miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na kutokuwa sawa kwa baadhi ya vichocheo mwilini 'hormonal imbalance'.

Sababu nyingine za tatizo hili ni matatizo ya uvimbe kwenye mfuko wa uzazi 'fibroid', lakini pia hali huweza kumkumba mwanamke mwenye historia ya kutoa kwa mimba mara kadhaa.

Lakini pia tatizo hili huweza kuchangiwa na matumizi ya baadhi ya dawa, hususani pale muhusiaka anapokuwa ametumia bila kupata ushauri wa wataalam.

Tatizo hili linapokuwa kubwa sana huweza kuathiri shughuli za mhusika za kila siku na hata kumtoa mhusika katika hali ya utulivu 'good mood' lakini mbaya zaidi huweza kumuingiza mhusika kwenye matatizo ya anemia.

Sasa kama wewe ni mwanamke ambaye unasumbuliwa na tatizo hilo unaweza kutumia mdalasini kama suluhisho la hali hiyo. Unachopaswa kufanya ni kupata unga wa mdalasini kijiko kimoja na kisha weka kwenye maji ya moto glasi moja kisha changanya vizuri.

Baada ya huo mchanganyiko kukaa kwa muda wa dakika 10 hadi 15 utachanganya na asali kijiko kimoja kisha changanya kwa pamoja na unywe.Unaweza kunywa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.

Ni vyema ukawasiliana nasi kwa maelezo zaidi kama unahitaji kutumia tiba hii, Mpigie Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment