Thursday, 12 November 2015

NDIZI NA UWEZO WAKE WA KUTIBU TATIZO LA UKAVU WA NGOZITatizo la ukavu wa ngozi ni moja ya mambo ambayo huwakabili baadhi ya watu na kuwafanya kukosa muonekano mzuri wa ngozi.

Miongoni mwa sababu za tatizo hili ni pamoja hali ya joto kali au mtu mwenye tatizo la kutapika tapika mara kwa mara au kuharisha huweza kukumbwa na tatizo hili.

Mtu yeyote huweza kupatawa na tatizo hili la ukavu wa ngozi pasipo kujalisha jinsia au umri, lakini watoto wadogo na wazee huweza kuwa katika hatari zaidi.

Sasa ili kukabiliana na tatizo hili jambo la kwanza unatakiwa kuanza kunywa maji ya kutosha zaidi ya unavyokunywa sasa.

Jifunze kunywa maji hata kama hauhisi dalili ya kubanwa na kiu na kwa mujibu wa watalaamu wa afya wanashauri mwanaume anywe glasi 13 kwa kila siku, huku mwanamke akinywa glasi 9 hadi 10.

Maziwa mtindi nayo huweza kuwa msaada mkubwa kwa wale wenye tatizo hili, hivyo unashauriwa angalau kupata kikombe kimoja cha maziwa mtindi kila siku ili kuimarisha afya ya ngozi yako zaidi.

Matumizi ya ndizi nayo ni muhimu sana kwa mtu mwenye tatizo hili la kupauka kwa ngozi, hii ni kwa sababu tatizo hilo huchangiwa na ukosefu wa madini mbalimbali hasa yale ya pottasium ndani ya mwili, hivyo ndizi huwa na madini hayo ambayo husaidia kurejesha unyevunyevu kwenye ngozi. Jitahidi ule ndizi moja hadi mbili kwa siku.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment