Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 3 November 2015

RIPOTI KUHUSU MVUA ZILIZONYESHA JANA JIJINI MWANZAMvua kubwa imenyesha mkoani Mwanza, na kusababisha maafa, ikiwemo vifo vya watu wawili

Mwanza,  hizo zimesababisha watu wawili kupoteza maisha kutokana na kusombwa na maji ya mvua iliyonyesha jana.

Aidha, mvua hizo zimesababisha kufungwa kwa muda uwanja wa ndege wa Mwanza kutokana na kujaa maji.

Mvua hizo zinasadikiwa ndiyo mwanzo wa El-Nino kutokana na taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kueleza jana kwamba, kutakuwa na mvua za El-Nino, kama ilivyokuwa imeelezwa katika taarifa yake ya Septemba mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo katika mkutano wake na waandishi wa habari, alisema mmoja wa waliopoteza maisha, ni mwendesha bodaboda wa Kirumba aliyekuwa amepakiza wanafunzi wawili akiwapeleka shuleni.
Maji yalifika hadi ndani

‘Leo (jana) saa 12 hadi saa 3 asubuhi Mwanza kulikuwa na mvua kubwa maeneo ya Kirumba… dereva wa bodaboda akiwa amewapakia wanafunzi wawili maji yaliwazidi na kwa bahati nzuri wale wanafunzi wanafunzi wawili waliokolewa lakini dereva bodaboda alisombwa pekeyake, mwili wake ulikutwa akiwa amefariki na pikipiki yake imepatikana‘  alisema Kamanda Charles Mkumbo.

Kuhusu uwanja wa ndege, mvua hizo zilisababisha kufungwa kwa saa tano kwa uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kujaa maji. Meneja wa uwanja wa Ndege wa Mwanza, Esther Madale alimwambia mwandishi wa habari hizi kwamba uwanja huo ulilazimika kufungwa kwa saa tano kwa ajili ya kuwezesha wahandisi, kufanya uchunguzi wa miundombinu yake.

Hakuna ndege iliyoruhusiwa kutua katika muda huo. “Ni kweli tulikumbwa na mkasa huo wa mvua ambazo zilinyesha mfululizo na kusababisha kufungwa kwa uwanja kwa muda…kwa sasa tunavyoongea tayari huduma zimerejea katika hali yake ya kawaida,” alisema Madale.

Uwanja huo wa ndege upo katika matengenezo makubwa, ikiwamo mnara wa kuongozea ndege, njia za kurukia ndege ambazo sasa ni meta 2000 na zinaongezwa hadi kufikia meta 3300. Ukarabati huo ulianza mwaka 2012 na ulitarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu.


Picha zote kwa hisani ya mwanzayetu.blogspot.com

No comments:

Post a Comment