Thursday, 5 November 2015

SAA MOJA YA MAZUNGUMZO YA RAIS KIKWETE NA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD IKULU (VIDEO)RAIS Jakaya Kikwete jana alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Civic United Front (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Itakumbukwa kwamba Maalim Seif pia alikuwa mgombea urais wa Zanzibar wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 25, lakini ukafutwa siku tatu baadaye na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Wakiwa kwenye picha ya pamoja
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, viongozi hao wawili walikutana kwa kiasi cha saa moja Ikulu, kuzungumzia hali ya kisiasa Zanzibar kufuatia ombi la Maalim Seif kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Kikwete.


“Viongozi hao wamekubaliana kuwa mashauriano yaendelee kufanyika baina ya pande zote zinazohusika na hali ya kisiasa Zanzibar,” ilieleza taarifa ya Ikulu. 

No comments:

Post a Comment