Wednesday, 4 November 2015

SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU TAARIFA ZA KUFARIKI KWA RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILIAM MKAPA

Kufuatia kuwapo kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kufariki dunia, imemlazimu Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene kutoa taarifa kuhusu habari hizo zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na kusema Rais Mkapa yupo salama.

Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua. 

Aidha, Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hususani Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotoshaji.
 
“Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” alisema Mwambene. 

Mwambene amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.
 
“Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” alisema Mwmbene, huku akiongeza kuwa Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka. 

Pamoja na hayo, Mwambene amevitaka vyombo vya habari kufanya kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi  iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao

No comments:

Post a Comment