Saturday, 14 November 2015

TAARIFA KUHUSU MADUKA YA DAWA YALIYO JIRANI NA HOSPITALI KUFUNGWA!!

Ishu ya uwepo wa maduka ya madawa kuwa jirani kabisa na hospitali imekuwa ikizungumzwa sana na wananchi wengi, huku wengi wao wakionekana kulalamikia utaratibu huo kutokana na baadhi ya wauguzi kuwaelekeza wagonjwa kufuata dawa kwenye maduka yaliyopo nje ya hospitali.

Kufuatia hali hiyo Msemaji wa Wizara  ya Afya na Ustawi wa Jamii Nsachris Mwamwaja amezungumzia moja ya mikakati ya Wizara hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na maduka ya dawa ndani ya hospitali ambayo yatakuwa ya Serikali chini ya Bohari kuu ya dawa MSD.

“Hospitali ya Muhimbili ina maduka ya dawa ndani, tumepanga kuhakikisha kila hospitali ya Serikali inakuwa na duka ndani, na tutahakikisha dawa zote zitakuwepo, lengo ni kuondoa malalamiko ya watu kuwa yale maduka ndio chanzo cha kukosekana kwa dawa mahospitalini” alisema Nsachris Mwamwaja

Katika hatua nyingine alisema “Ni kweli haya maduka yapo sehemu ambazo wauguzi ndio hutoa maelezo wagonjwa wakanunue hizo dawa katika maduka hayo, wagonjwa wanaotumia huduma za mifuko ya jamii pia watakuwa wakitumia maduka ya hospitali za Serikali, nia yetu ni wagonjwa wapate dawa bila usumbufu wowote”.

Msemaji huyo pia alieleza kuwa kwa sasa wapo katika mazungumzo na wahusika kuhusu zoezi hilo na kudai kwamba litafanyika bila kutumia nguvu na badala yake watafanya mazungumzo ya maelewano kati ya wizara na wafanyabiashara wa maduka hayo ya dawa ambayo yapo karibu na hospitali.

"Lazima tuwe na maelewano na watu waelewe kwanini hiki kitu kinafanyika isiwe tu juu juu, watu waelewe kwa undani hata wale wenye maduka walielewe hilo na wajue kwanini tunawaondoa maeneo ya hosipitali kwahiyo siyo zoezi la kumuumiza mtu lakini ni zoezi la kufanya huduma ziende vizuri na kila mwananchi afaidike na hizi huduma. " alifafanua Mwamwaja

Mbali na hayo Wizara hiyo ilieleza kuhusu uwepo wa wimbi la utapeli ambao umekuwa ukifanywa kwa waajiri ambapo wamejitokeza matapeli na kuwapangia watu maeneo ya kwenda kufanya kazi kitu ambacho si kweli kwa kuwa Wizara hiyo haijatoa majina ya ajira na haijawapangia watu vituo vya afya.

“Kuna taratibu za kukufanya uingizwe kwenye mfumo wa kulipwa na Wizara, ni ngumu kuingia kirahisi huo ni udanyangifu unaofanywa na baadhi ya watu ambao si waaminifu katika baadhi ya ofisi..pia wizara haitoa barua wala kuajiri bali inatoa majina na kupeleka kwa waajiri husika;

No comments:

Post a Comment