Thursday, 19 November 2015

TABIA HATARI ZINAZOWEZA KUMFANYA MWANAUME KUSHINDWA KUMPATIA MWANAMKE MIMBA


Naamini kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii basi utakumbuka kwamba tayari tumezungumza kuhusu matatizo ya uzazi kwa kina baba na namna tatizo hilo linavyojitokeza kwao

Kwa sasa napenda kukwambia baadhi ya mambo ambayo yakifanywa na wanaume basi huweza kuwaweka katika hatari zaidi ya kuingia kwenye tatizo la ugumba au kushindwa kutungisha mimba kwenye ndoa zao.


Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na suala la uvutaji sigara au matumizi ya madawa ya kulevya hii ni moja ya chanzo ambacho huwez kumuingiza mwanaume kwenye matatizo ya kushindwa kutungisha mimba.

Unapotumia sigara au aina yoyote kwa muda mrefu huchangia kupunguza uzalishaji wa mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa

Unywaji pombe, mwanaume anayekunywa pombe kupita kiasi huwa katika hatari kubwa ya kuzingwa na tatizo hili kwani unapokunywa pombe husababisha uzalishaji wa mbegu za kiume kushuka na kutokuwa na ubora wa kutosha.

Uzito kupita kiasi huweza kuwa chanzo cha tatizo hili kwa wanaume, hivyo ni vyema kuzingatia uzito wa mwili unakuwa wa kawaida na hii huwezekana endapo utakuwa ni mtu wa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho vya kutosha huchangia sana tatizo hili, hivyo ni muhimu kupata mlo kamili kila siku na kuhakikisha unapata chakula chenye virutubisho muhimu kama vile vitamin C ya kutosha na madini ya zinc pia. 

Mwili unapoapta vitamin C ya kutosha na madini ya zinc basi humsaidia sana mhusika yaani mwanaume kuwa na uwezo mzuri wa mbegu kusafiri au kuogelea vizuri.

Hayo ni machache tu kuhusu tatizo hili la uzazi kwa kinababa kama utakuwa na swali au maoni wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment