Monday, 2 November 2015

TATIZO LA HARUFU MBAYA SEHEMU ZA SIRI HUWATESA SANA WANAUME, TUJIFUNZE NAMNA YA KUKABILIANA NALO HAPAKwa kawaida wanawake wengi hudhani kuwa na tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni husababishwa na matokeo ya uchafu na kutojisafisha vizuri.

Pale inapotokea mwanamke akawa na tatizo hili wanaume ni moja ya watu ambao hukwazika zaidi na wengine hufikia hatua hata ya kuvunja mahusiano

Hata hivyo wanawake wengi kuamini kwamba tatizo hilo hutokana na kuwa na hali ya uchafu sehemu zao za siri wengi wao huamua kuanza kujisafisha vizuri na kwa juhudi zaidi hali ambayo husababisha kuongezeka kwa tatizo zaidi.

Ukweli ni kwamba unapojisafisha zaidi ndiyo unaongeza tatizo badala ya kutatua, licha ya kwamba kweli kuna ukweli ndani yake kuwa uchafu huweza kusababisha harufu mbaya sehemu za siri.

Kwa asilimia kubwa tatizo hili husababishwa na vijidudu yaani bakteria  kwa asilimia kubwa.

Kwa asili sehemu za kike za siri huishi jamii ya bakteria wiitwao  lactobacillus ambao jukumu lao kubwa ni kufanya mazingira ya sehemu hiyo kuwa katika hali nzuri, hata hivyo kutokana na njia mbaya za kusafisha uke hasa kujisafisha kupindukia ama kwa kutumia sabuni zenye dawa,  husababisha bakteria hawa kufa kwa wingi na nafasi yake kuchukuliwa na aina nyingine ya bakteria  ambao huzaana kwa wingi na hivyo kusababisha  tatizo hilo.

Pia kwa wale ambao wanajamiana kinyume na maumbile wao huweza kuwa katika hatari kubwa ya kuhamisha bakteria wanaoishi kwenye nji ya haja kubwa na kuwahamishia ukeni, ambapo huzaliana na kusababisha madhara.

JINSI YA YA KUJIKINGA 
Acha kuosha sehemu za siri za kike kupita kiasi kwani husababisha kuondoa vijidudu wa asili wa sehemu hizo (lactobacilli) na kukaribisha bakteria wenye madhara.

Pia epuka matumizi ya sabuni zenye dawa kila unaposafisha sehemu zako za siri za kike, kwani sabuni hizo nazo huchangia kuua bakteria wa asili wa sehemu hizo za siri. Hii haimanishi kuwa usiwe unasafisha sehemu zako za siri kumbuka usafi pia ni muhimu kwni uchafu hukaribisha vimelea vya magonjwa.

Ikiwa tayari unatatizo hilo ni vyema ukafanya utaratibu wa kuonana na wataalam wa tiba ili kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kujua sababu za tatizo lako.

Kumbuka kujisafisha sana si suluhisho la tatizo kwani huweza kuongea ukubwa wa tatizo zaidi badala ya kuwa suluhisho.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment