Saturday, 7 November 2015

TATIZO LA NGIRI (HERNIA) HUWAKOSESHA RAHA SANA WANAUME, ZIFAHAMU SABABU ZAKE NA NAMNA YA KUEPUKAHabari za leo Jumamosi mdau wangu wa www.dkmandai.com leo napenda kuzungumzia tatizo la ngiri (hernia) 

Nimeona ni muhimu kuzungumzia tatizo hili baada ya kupokea ombi kutoka kwa mdau wetu anayeitwa Peter Mayanga ambaye aliwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic -mhc.

Hivyo naomba nianze kwa kusema kuwa ugonjwa wa ngiri hujitokeza pale inapotokea sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa tumbo na kuingia katika korodani moja au sehemu ya juu ya paja.

Ngiri ni hali ambayo husababisha maumivu makali sana kwa mhusika na mara nyingi matibabu yake huhitaji upasuaji.

Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote na miongoni mwa sababu ambazo huweza kumfanya mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, ukosefu wa protini za kutosha mwilini, kufanya kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito nayo huweza kuwa sababu, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu.

Wengi wa waathirika wa tatizo hilo hufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea.Pia inashauriwa kufanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii husaidia kuwa vizuri.

Kama unaswali au ushauri au unasumbuliwa na tatizo hili (ngiri) unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia kama unapenda kutuambia somo gani tuandae tena kwaajili yako kupitia tovuti hii basi tutumie sms kupitia ukurasa wetu wa facebook wa Mandai Herbalist Clinic -mhc nasi tutayafanyia kazi mawazo yako.

No comments:

Post a Comment