Wednesday, 18 November 2015

TIBA ASILI YA MAFINDOFINDO (TONSILLITIS) HII HAPAMafindofindo tonsillitis ni ile hali ya kuatwa na michubuko au kuhusi maumivu kwenye kinywa hususni pale unapomeza chakula au kunywa kinywaji chochote.

Tatizo hili huweza kuchangiwa na unywaji wa maji ya baridi kupita kiasi, licha ya kwamba hiyo si sababu pekee ya tatizo hilo kwani huweza kuchangiwa na vumbi, pamoja na ulaji wa vitu vikali kama pilipili.

Wakati unapokuwa na tonsil unashauriwa kuepuka kabisa matumizi ya maji baridi  na vitu vyote vikali na badala yake kutumia maji ya moto au ya kawaida

Ili kukabiliana na tatizo hilo pale unapopatwa na mafindofindo utahitajika kutumia maji ya uvuguvugu pamoja na kiasi cha chumvi kisha utaweka mdomoni na kusukutua mara 4 kwa siku, huku ukihakikisha maji yanafika kooni kabisa.

Pia mdalasini huweza kuwa msaada wa tatizo hili unachopaswa kufanya ni kupata ungawa mdalasini kijiko kimoja weka kwenye glassi ya maji kisha changanya na asali vijiko viwili baada ya hapo changanya mchanganyiko wako vizuri kisha kunywa mara mbili kwa siku kwa muda wiki moja.

Ukiona hali inaendelea basi ni vyema kufika kwenye kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi, pia unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

2 comments:

 1. Doctor habar yako.
  mm pia nasumbuliwa na hayo maradhi na nilikwend spital nikapatiwa dawa .
  tatizo lakn bado lipo.
  na nimefanya kam kuvimba ndani ya kinywa na pia ukiangalia kinywa karibu na kidaka tonge utakuta
  kama kuna usaha usaha hivi.
  tatiz n hilo ama laaa.

  ReplyDelete
 2. Asante kwa ushauri Wako mungu akubariki sana

  ReplyDelete