Monday, 23 November 2015

UMUHIMU WA CHAKULA BORA KATIKA KUTUEPUSHA NA SUMU MWILINIAfya zetu ni muhimu kuzingatiwa kila siku na namna ya kuzingatia ni kuhakikisha unakula vizuri yaani kwa kufuata kanuni za kiafya na lishe bora pia.

Ni wazi kwamba katika maisha yetu kuna wakati huwa tunakula na kunywa vitu ambavyo huweza kuwa sumu ndani ya miili yetu na hivyo kuupa mwili wetu shughuli nzito zaidi ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Kimsingi tunaposema sumu hatuna maana ile sumu ya kuua panya au mende bali sumu mwilini ni kitu chochote ambacho huhatarisha utendaji kazi wa mifumo au viungo vya mwili ndani ya mwili na huweza kupelekea kifo.

Kuna aina mbili za mwanadamu kupokea madhara ya sumu mwilini kwanza ni kupitia vitu ambavyo vipo nje ya mwili, binadamu huvitumia na matokeo yake humuathiri. 

Vitu hivyo mtu huweza kuvitumia kwa kujua au kutokujua kuwa kwake ni sumu, mfano Sumu nyingine hujitokeza kwa kukosa au kutozingatia maelekezo ya matumizi ya dawa tunayopewa na wataalam wa afya.

Kuna njia kadhaa za kupunguza sumu mwilini ikiwa ni pamoja na matumizi ya chakula bora yaani ni vile vyakula vyenye virutubisho ambavyo huvunja vunja na kuondoa sumu mwilini, vyakula hivyo huulinda mwili dhidi ya kemikali hatarishi zinazozalishwa mwilini. 

Virutubisho hivi ni pamoja na Vitamin A, Vitamini C na Vitamini E. Vitamini hizi hupatikana katika mboga za majani na matunda, mfano mchicha, spinachi, karoti, machungwa, nanasi, maembe, pamoja na mafuta ya mimea mfano alizeti nk.

Ili miili yetu iweze kufanya kazi vizuri na tuendelee kuwa na afya njema, inabidi tuepukane na sumu hizi, pale inapo tulazimu zitumike (mfano zebaki, migodini), basi tuzidishe umakini katika kujilinda afya zetu, na pia tubadilishe aina ya maisha au ulaji wa vyakula, matunda na mboga za majani ni walinzi wakubwa sana wa afya zetu.


Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment