Wednesday, 18 November 2015

VIFAHAMU HIVI VYAKULA MUHIMU KWA MAMA ALIYEJIFUNGUA


Mara nyingi mama mjamzito anapojifungua huhitaji uangalizi wa karibu zaidi ili kuweza kurejesha afya, lakini pia na nguvu ndani ya mwili na vyote hivyo huwezekana endapo mama atapata mlo kamili.

Ninavyo hapa baadhi ya vyakula ambavyo ni muhimu kupatikana kwa mama aliyetoka kujifungua vyakula vyenyewe ni kama hivi vifuatavyo>>>>

Mayai
Mayai
Mayai ni muhimu sana kwa mama aliyejifungua kwani yana virutubisho mbalimbali kama vile protini ambayo husaidia sana kumuongezea mama nguvu za kuweza kujihimili yeye mwenyewe pamoja na kuweza kumuhudumia mtoto.

Mboga za Majani
Spinach / chainizi
Aina yoyote ya mboga ya majani ni nzuri kwa mama aliyetoka kujifunguaa, lakini spinach ni nzuri zaidi kwani ina vitamini  A nyingi zaidi ambayo ni nzuri kwa mama na mtoto.

Lakini pia spinach ina folic acid ambayo ni chanzo kizuri cha seli za damu mwilini ambayo ni muhimu sana kwa mama ambaye amepoteza damu nyingi wakati wa kujifungua, lakini pia husaidia kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa kwa mama.

Spinach pia ina madini ya manganese ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa, lakini ni vyema ikakumbukwa kwamba mboga hizi za majani ni vyema zikatumika kama salad au supu bila kuweka kiungo chochote ili kupata virutubisho vizuri zaidi.

Maziwa.
Maziwa
Lishe ya mama aliyetoka kujifungua inahitajika kuwa na maziwa pia kwani husaidia sana uzalishaji wa maziwa kwaajili ya kummypmyesha mtoto.

Maziwa yana vitamin D na B pamoja na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto.

Ndani ya maziwa pia kuna madini ya calcium yakutosha ambayo humsaidia mama kurejesha madini hayo ambayo hupotea wakati wa kipindi cha kunyonyesha, lakini pia maziwa yatamsaidia mama kuondokana na kuwa na ngozi kavu. Hivyo ni vizuri mama aliyejifungua akapata glasi mbili za maziwa kila siku.

Hayo ni kwa uchache tu kuhusu lishe na vyakula ambavyo huweza kula mama baada ya kujifungua kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment