Saturday, 21 November 2015

VITU MUHIMU AMBAVYO VITAKUFANYA KUENDELEA KUONEKANA KIJANA KATIKA MAISHA


Siku zote kila mtu hupenda kuendelea kuonekana vizuri na kuwa na sura inayoendana na umri alionao.

Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu muonekano wao na umri walionao huonekana ni tofauti kuna baadhi muonekano wao ni mkubwa kuliko umri wao na kuna wengine muonekano wao ni mdogo kuliko umri pia jambo ambalo kwakiasi kikubwa huwa si tatizo.

Shida huwa inakuja pale ambapo umri wa muhusika hauendani kabisa na sura yaani miaka michache na muonekano wa sura ni wa kikubwa zaidi.

Sasa kuna baadhi ya vyakula ambavyo humsaidia mhusika kubaki na muonekano unaofanania na umri wake 'anti-aging superfood'

Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na mboga za majani hususani spinach, mboga hii inavirutubisho vingi kama vitamin C na E pamoja na kirutubisho kiitwacho beta-carotene ambavyo kwa pamoja hulinda ngozi dhidi ya miale hatari ya jua.

Mafuta ya mzaituni nayo ni mazuri sana kwa kuimarisha afya ya ngozi na kumfanya mhusika kuendelea kuonekana kijana muda wote wa maisha yake kwani ndani ya mafuta hayo kuna vitamin A, E ambazo ni muhimu sana kwa kuimarisha afya ya ngozi.

Hayo ni machache tu kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment