Friday, 27 November 2015

VITU MUHIMU VYA KUTUMIWA NA MTU ALIYEATHIRIKA NA MATATIZO YA UVUTAJI SIGARA


Habari za leo wadau wa www.dkmandai.com karibuni tuendelee kufahamishana mambo mbalimbali kupitia tovuti yetu hii.

Leo napenda kuzungumza na wale wapenzi wa kuvuta sigara, hii ni moja ya tabia ambayo wengi wanayo na wengi wanavuta licha ya kwamba wanatambua madhara ya kuvuta sigara

Sasa leo nimeona nitoe somo kidogo la namna ya kuondoa sumu mwilini iliyotokana na moshi wa sigara 'nicotine.'

Kwanza kabisa ili kuondoa sumu hii itokanayo na moshi wa sigara muathirika anapaswa kunywa maji ya mengi zaidi kila siku, kuanzia glass nane hadi kumi na mbili kwa siku.
Kunywa maji ya kutosha
Unywaji wa maji ya kutosha utasaidia sana kuondoa sumu za moshi wa sigara mwilini kupitia kwenye ngozi kwa kutoa jasho.


Chungwa
Machungwa nayo ni sehemu ya tunda lenye nafasi nzuri ya kumaliza sumu itokanayo na moshi wa sigara 'nicotine' Sababu inayofanya tunda hili kuwa na uwezo wa kutoa sumu hiyo ni kutokana na uwingi wa vitamin C inayopatikana ndani ya chungwa ambayo husaidia kuzalisha metabolism ambayo mwisho wa siku hufanya kazi ya kuflashi sumu mwilini.


Juisi ya karoti nayo hapa inasimama kama moja ya njia ya kuondoa sumu ya moshi wa sigara mwilini, kutokana na juisi hiyo kuwa na vitamin A, B, C, K ambazo husaidia kumaliza sumu hatari itokanayo na sigara.


Juisi ya karoti
Kwa kawida sumu ya nicotine  huharibu ngozi, lakini kwa sababu juisi ya karoti huwa na vitamin muhimu kwa ngozi basi juisi hii hufaa zaidi kuepukana na uharibifu huo.

Broccol
Broccol hii ni aina fulani ya mboga ambayo mara nyingi hupendelewa sana kutumiwa na wenzutu wahindi, ndani ya broccol kuna vitamin B5, C.
Ndani ya 'broccol' kuna malighafi muhimu sana ambayo husaidia kulinda mapafu kutoharibika kirahisi na sumu hiyo ya sigara. 

Mbali na hayo, pia spinach ni nzuri kwa kumaliza sumu ya moshi wa sigara mwilini kutokana na kuwa na vitamin pamoja na 'folic acid' 


Mboga ya Spinach
Hizo ni mbinu za kuweza kukusaidia kuondoa sumu hatari zilizosababishwa na matumizi ya sigara, lakini ni vyema kuachana kabisa na matumizi ya sigara kwani ni hatari sana kwa afya yako.

Kwa ushauri maoni unaweza kutupigia simu kwa namba zifuatazo 0769 400 800, 0784 300 300, 0716 300 200 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment