Friday, 13 November 2015

VYAKULA VYA KUEPUKA KULA USIKU KABLA YA KULALA

Uchunguzi wa kitaalamu unaoneesha kuwa watu wanene wapo katika hatari ya kupata maradhi ya kiharusi, kisukari na magonjwa ya moyo.

Kufahamu umuhimu wa chakula na wakati sahihi wa kula ni muhimu sana kwani kuna baadhi ya watu hawafahamu matumizi ya baadhi ya vyakula na kutokujua chakula gani wale na kwa wakati gani.

Wataalamu wa masuala ya afya na lishe wanaeleza kuwa baadhi ya vyakula vikiliwa usiku husababisha athari kwa afya za watumiaji wake.

Miongoni mwa athari  hizo ni pamoja na kuongezeka kwa uzito bila mpangilio, mhusika kukosa usingizi na kulala fofo kutokana na tumbo kujaa.

Pia wengine huweza kulala kwa usingizi wenye kukatikakatika, lakini hapa kuna orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo si vizuri kula wakati wa kwenda kulala kwa watu wanene na wenye uzito mkubwa.

Nyama Nyekundu
Kula nyama nyekundu usiku huweza kumfanya mhusika asipate usingizi mzuri kwa kuwa tumbo hushindwa kusaga vyakula vigumu uwapo usingizini.

Kama itakuwa ni ngumu lazima kula nyama, basi ni vyema ukala  nyama nyeupe kama vile kuku au samaki.

Vyakula vyenye Mafuta Mengi
Hivi ni aina ya vyakula huweza kukusababishia kuhisi uchovu na uvivu katika siku inayofuata.

Kwa maelezo zaidi wasiliama nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment