Saturday, 28 November 2015

YAFAHAMU HAYA MAAJABU YA APPLE LA KIJANI KATIKA TIBA


 Desktop Wallpaper · Gallery · Windows 7 
 Green apples
Habari za leo Jumamosi mdau wa www.dkmandai.com naamini utakuwa upo vizuri weekend hii.

Kama ilivyo kawaida yetu kila siku huwa tunaelezana faida mbalimbali za matunda pamoja na mimea tiba kwa ujumla wake na leo napenda kuzungumzia kuhusu faida za apple za kijani au tufaa la kijani.

Ukweli ni kwamba mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu tunda hili lakini ni vyema ikafahamika kuwa kuna utofauti wa virutubisho kati ya tufaa la kijani 'green apple' na yale matufaa mekundu.

Sasa leo tuangazie kuhusu faida zinazopatikana kwenye apple la kijani kama ifuatavyo>>>

Kwanza kabisa tunda hili lina sifa ya kusaidia kuimarisha afya ya macho kutokana na kuwa na vitamin A nyingi ambayo husaidia sana pia kuimarisha afya ya mifupa.

Aidha, matumizi ya apple la kijani pia ni chanzo kizuri cha nguvu mwilini kwani ndani yake kuna vitamin B1 ambayo husaidia kubadili carbohydrate kuwa nishati mwilini 'energy'

Matumizi ya mara kwa mara ya apple la kijani husaidia kumkinga mhusika dhidi ya magonjwa yasiyoaambukizwa kama vile kiharusi kwani ndani ya tunda hili kunamadini yenye nguvu ya kupambana na cholesterol.

Faida nyingine ya tunda hili ni kupambana na kuvuja kwa damu mwilini, hii ni kutokana na kwamba apple la kijani huwa na vitamin K za kutosha na hivyo kusaidia sana tatizo la uvujaji damu jambo ambalo lisipopewa umaanani huweza kusababisha hata kifo.

Pia tunda hili hurahisisha umeng'enyaji wa chakula mwilini kwani tunda hili lina nyuzinyuzi 'fiber' za kutosha jambo ambalo pia husaidia kuzuia tatizo la kukosa choo kwa mhusika 'constipation'

Hayo ni machache kuhusu tunda hili kwa mengine mengi zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment