Wednesday, 18 November 2015

YAFAHAMU HAYA MAMBO MUHIMU KUHUSU UGONJWA WA KIFAFAKifafa ni ugonjwa unaosababishwa na matatizo katika mfumo wa fahamu ya mwili na mara nyingi ugonjwa huu huambatana na mhusika kuanguka huku akitetemeka na mara nyingine hutokwa na povu mdomoni au kutokwa na haja ndogo (mkojo) bila kujitambua kujielewa na oia mgonjwa huweza kung’ata midomo au ulimi pale anapokumbwa na tatizo hili.

Kimsingi chanzo cha ugonjwa huu hakifahamiki vizuri kitaalamu lakini miongoni mwa vihatarishi au mambo yanayoweza kumfanya mtu apate ugonjwa huu ni pamoja na kuwa na historia ya kifafa katika familia yaani (Kurithi), matatizo ya mishipa ya damu katika ubongo, maambukizi katika ubongo mfano homa ya uti wa mgongo, mtoto kuzaliwa kabla ya umri wake,

Chanzo kingine ni ajali mbaya katika eneo la ubongo, kukosekana kwa hewa ya kutosha katika ubongo, mtoto kupatwa na degedege mara kwa mara katika miezi ya mwanzo ya kuzaliwa kwake, uvimbe katika ubongo na sababu nyinginezo.

Pamoja na visababishi hivyo hapo juu, wakati mwingine kumekuwepo na vitu vinavyochochea mtu apatwe na dalili hizo (kuanguka kifafa), mfano wa vichochezi ni pamoja na kutokula vizuri, hali ya hewa, msongo wa mawazo pamoja na mazingira yenye kelele.

Utambuzi wa kifafa hufanyika kitaalamu kwani siyo kila mtu anayeanguka na kutetemeka basi huwa na kifafa, inawezekana likawa ni tatizo lingine. hivyo ni vyema kuwaona wataalam inapotokea tatizo hili.

Mtu mwenye kifafa huweza kukumbwa na madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupoteza viuongo vyao muhimu ikiwa pale atakapoanguka ataumia, hivyo ni vizuri pale unapojihisi kuwa na tatizo hili ukawashirikisha ndugu na jamaa zako wa karibu kwa lengo la kupata ufumbuzi wa tatizo lako.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300  au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment