Wednesday, 11 November 2015

YAFAHAMU HAYA MAMBO MUHIMU YATAKAYOENDELEA KUIMARISHA AFYA YAKO KILA SIKU


Katika maisha kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kuendelea kuimarisha afya za miili yetu, leo kutoka 'Mandai Health Tips'   nimeona nikupe haya mambo mawili muhimu kwako mdau wangu.

Kwanza amua kuwa mtu wa mazoezi, unaweza kuondoka kila siku asubuhi unapoamka na kuanza mazoezi.

Mazoezi hayo yanweza kuwa ya kukimbia taratibu, kutembea angalau kwa dakika 15 au amua kutembea kila siku ili kuufanya mwili utoke jasho.

Kwa kufanya mazoezi mara kwa mara utakuwa unafanya kazi ya kuondosha collestrol mwilini yaani yale mafuta mabaya mwilini ambayo huenda kuganda kwenye mishipa ya damu  jambo ambalo ni hatari, lakini unapofanya mazoezi mafuta hayo hutoweka.

Pia kwakufanya mazoezi humsaidia mhusika kumuepusha na uwezekano wa kukumbwa na shinikizo la damu au matatizo ya moyo.

Jambo la pili muhimu ni kunywa maji, ili uwe na afya nzuri na bora ni vyema ukajitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku.

Inashauriwa angalau kwa siku unywe glasi nane hadi kumi na sita kwa, anza asubuhi mara unapoamka na unywe glasi 2 hadi 5.

Mchana wote endelea lakini usinywe maji wakati wa kula chakula, unaweza kunywa maji dakika kadhaa kabla ya kuanza kula au mara baada ya kula chakula.

Maji huusaidia mwili kutoa taka mwili (sumu) kwa njia ya jasho au haja ndogo, hivyo ni vyema ukaweka kawaida ya kunywa maji mara kwa mara kama unapenda kuonekana mwenye afya nzuri.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment