Monday, 9 November 2015

ZIARA NYINGINE YA GHAFLA ALIYOIFANYA LEO RAIS MAGUFULI KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILIRais wa Tanzania Dk.John Pombe Maguli amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

Inaelezwa kwamba hali iliyokuwepo leo Muhimbili haikuwa tofauti sana na ile hali aliyoikuta wakati alipotembelea Wizara ya Fedha baada ya kukuta baadhi ya watumishi kutokuwepo eneo la kazi bila taarifa rasmi.

Hii ni mara ya pili sasa kufanya ziara za ghafla tangu Mheshimiwa  Dk Magufulu aingie Ikulu ambapo ya kwanza ilikuwa ni ile aliyofanya Wizara ya Fedha na kukuta baadhi ya wafanyakazi hawapo wakati ulikuwa ni muda wa kazi

Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Aga Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Dr Helen Kijo-Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment