Tuesday, 3 November 2015

ZIFAHAMU HIZI FAIDA ZA KUNYWA JUISI YA TIKITI MAJI KIAFYA

Habari za Jumatano ya Novemba 4, 2015, asante sana kwa kuendelea kuwa karibu nasi www.dkmandai.com na kujipatia taarifa mbalimbali kutoka kwetu.

Leo ninayo furaha kukupa baadhi ya faida za matumizi ya juisi ya matikiti maji, hii ni moja ya juisi ambayo wengi wetu hatuna utamaduni sana wa kuitumia wala kufikiria kuitengeneza majumbani mwetu, lakini huenda leo ukizijua hizi faida utaanza kuipenda.

Kwanza kabisa ni vyema ifahamike kuwa juisi ya tikiti maji inauwezo wa kuzuia magonjwa mbalimbali, miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na yale ambayo si ya kuambukiza kama vile pumu, kiharusi pamoja na matatizo ya moyo hasa mshtuko wa moyo yaani 'heart attack' hii ni kutokana na uwezo wake wa kuweza kupambana na sumu 'cholesterol ' kwenye mishipa ya damu.

Unapokunywa glasi moja ya juisi ya tikiti maji kila siku basi tambua unajiweka katika nafasi kubwa ya kujiepusha na saratani ya tumbo, maumivu ya viungo yaani 'arthritis', pumu, lakini pia juisi ya tunda hili husaidia sana kwa wale wenye shida ya mawe kwenye figo.

Aidha, unywaji wa juisi hii ni sawa na kupata mlo kamili kutokana na kuwa na kiasi cha protini, sukari kiasi pamoja na madini.

Unapokunywa juisi ya tikiti maji ndani yake kuna madini ya 'potassium' ambayo husaidia sana kusawazisha mapigo ya moyo na pia madini hayo ya 'potassium' husaidia kuongeza uimara wa mwili.

Pia juisi ya tikiti maji humpatia mnywaji madini ya calcium ambayo husaidia kuimarisha afya ya mifupa mwilini, hivyo juisi hii inawafaa sana wazee pia.

Lakini pia mbegu za tikiti maji zimesheheni madini ya chuma 'iron,' hivyo itakuwa nzuri zaidi ikiwa utaamua kusaga mbegu hizo na kuzichanganya ndani ya juisi yako ya tikiti maji kwani kwa kufanya hivyo itakusaidia sana kuepukana na matatizo kama ya anemia.

Hizo ni faida kuhusu juisi ya tikiti maji, lakini kama utakuwa na swali lolote kuhusu tuliyoyazungumza hapo juu basi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa namba za simu zifuatazo, 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment