Tuesday, 17 November 2015

ZIFAHAMU HIZI SIFA ZA MBEGU ZA MABOGA KIAFYA

Mbegu za maboga zinafaida nyingi sana kiafya na hujumuisha kiwango kingi cha protini na vitamin, huku ikiaminika kwamba, mbegu hizo huweza kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu na jambo la msingi zaidi ni kwamba gramu moja ya mbegu za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ya maziwa.

Watu wengi wanaweza kudharau mbegu za maboga pengine kwa kutokufahamu faida zake, lakini wazi kwamba mbegu hizi ni miongoni mwa mbegu zenye faida kubwa mwilini, kwani huweza kuzuia na kutibu hata baadhi ya magonjwa hatari yaliyoshindikana hospitalini.

Miongoni mwa faida za mbegu hizi ni pamoja na kuimarisha mifupa na moyo, hii ni kutokana na kuwa na kiwango kingi cha madini aina ya magnesium, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na uimarishaji wa mifupa pamoja na mishipa ya damu.

Aidha, mbegu hizi za maboga pia zina kiwango cha madini aina ya 'zinc', ambayo faida yake mwilini ni pamoja na kuimarishaji kinga mwilini , Hali kadhalika zinc huimarisha nguvu za kiume.

Kutokana na kuwa na kiwango kingi cha zinc, tafiti zinaonesha kuwa mafuta ya mbegu zenyewe za maboga huweza kutumika kama dawa ya kutibu saratani ya kibofu.

Jinsi ya kutumia mbegu hizi utahitajika kupata kiasi cha mbegu za maboga kisha saga na utatumia unga huo kwa kuweka kwenye maji ya motoa ua uji. Tumia mara mbili kwa siku asubuhi na jioni


Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment