Monday, 7 December 2015

AINA TATU ZA VYAKULA NA MATUNDA MUHIMU KWA AFYA YAKO


Moja ya njia nzuri ya kuishi vizuri kwa afya ni pamoja na hii ya kula chakula bora na sahihi na kuzingatia kufanya mazoezi.

Leo tutagusia baadhi ya vyakula ambavyo vimekuwa vikitajwa kuwa ni vyakula bora, na vyenye faida nyingi kwa mlaji.

Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na samaki, ambapo huwa na virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo husaidia katika kuulinda moyo dhidi ya maradhi.

Aidha, samaki pia wanasifika kwa kuwa na virutubisho ambavyo humuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka pamoja na virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na saratani mwilini.

Hali kadhalika, ulaji wa samaki pia husaidia kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini, hivyo unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo.

Unapotumia samaki husaidia kumpatia mlaji virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na protini, vitamini B3, vitamin D, vitamini B6, Omega 3 Fatty Acids. nk

Karanga  nazo ni moja ya chakula chenye faida pia mwilini, miongoni mwa faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, kupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri.

Unaweza kupata faida za karanga kwa kutumia karanga zenyewe au siagi yake iliyotengenezwa kutokana na karanga. Unapopata karanga za kuchemshwa huwa nzuri zaidi.

Karoti pia imekuwa ikitajwa kuwa na faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushusha kolestro mbaya mwilini, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini.

Matunda ni muhimu sana kwa afya yako na miongoni mwa matunda muhimu mwilini ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha kamba lishe (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa sana mwilini.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300  300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment