Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 31 December 2015

BORESHA MFUMO WA MMENG'ENYO WAKO WA CHAKULA KWA KUTUMIA PILIPILI MANGA


 Pilipili manga ni mbegu ndogo ndogo ambazo ukiziangalia vizuri sana basi zinataka sana kufanana na mbegu za papai.

Rangi yake ni nyeusi hivi na ladha yake ni mfano wa pilipili.

Moja ya faida za kiungo hiki ni pamoja na kuongeza hamu ya kula, hivyo ni kiungo kizuri sana kwa wale wenye kukosa hamu ya chakula.

Aidha mbegu hizi za pilipili manga husaidia sana kuboresha mmeng’enyo wa chakula na hivyo kumfanya mhusika kuepuka tatizo la ukosefu wa choo ‘constipation.’

Pamoja na hayo, pilipili manga pia husaidia wale wenye shida ya kupata haja ndogo yenye kuambatana na maumivu makali na kutoka kwa taabu.

Pilipili manga, pia husaidia sana kuleta uoni mzuri kwa wale wenye uoni hafifu

Halikadharika pilipili manga husaidia sana kukabiliana na matatizo maumivu ya viungo, sambamba na kutibu magonjwa kinywa, fizi na meno.

Maoni yako au ushauri na maswali pia tunayapokea kupitia namba zetu za simu 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment